Jimmy Carter alikuwa rais wa kwanza wa Marekani kufanya ziara ya kiserikali barani Afrika chini ya jangwa la Sahara na kutangaza “kumalizika kwa siku mbaya kwa Marekani”.
Kushamiri kwa bara hilo ni mahali ambako urithi wa Carter kuhusu kazi za haki za binadamu bado zinaonekana sana. Marais wa awali walionyesha mtizamo mdogo kwa Afrika.
Carter alihamasisha demokrasia kote katika bara hilo na alikaribia kufanikisha azma yake ya kuondoa minyoo ya Guinea, kimelea ambacho kiliwaathiri mamilioni ya watu.
Waziri wa Afya wa Ethiopia anasema “Rais Carter alifanya kazi kwa ajili ya binadamu wote bila ya kujali rangi, dini au hadhi.” Ethiopia ina zaidi ya watu milioni 110, huku kesi moja ya minyoo ya Guinea ikiripotiwa mwaka jana.
Forum