Raia tisa wakiwemo wanawake na watoto waliuliwa katika shambulizi la kwenye gari katika mkoa wa Segou nchini Mali, kundi la kiraia na ushirika wa uasi wamesema Jumamosi jioni wakilishutumu jeshi la mamluki wa Russia.
Gari hilo lilikuwa likisafiri kutoka mji wa Nioni kwenda kambi ya wakimbizi ya nchini Mauritania siku ya Alhamisi wakati liliposhambuliwa amesema Mohamed Elmaoulod Ramadane, msemaji wa ushirika wa makundi ya Tuareg ambayo yanapigania uhuru wa eneo la Kaskazini mwa Mali.
Yeye na Kal Akal wa chama cha kiraia wamesema wanajeshi wa Mali na washirika wao wapiganaji kutoka kundi la binafsi la Wagner la Russia walifanya shambulizi hilo. Katika taarifa tofauti mkuu wa Kel Ansar moja ya makundi makubwa ya Tuareg, wametaka uchunguzi ufanywe lakini amesema wanajeshi wa Mali hawakuhusika na umwagaji damu huo.
Wapigana wa Wagner wamekuwepo nchini Mali tangu jeshi lilipokamata madaraka katika mapinduzi mawili mwaka 2020 na 2021 na kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa Mataifa.
Forum