Wanadiplomasia wakuu wa Mashariki ya Kati na Ulaya, Jumapili wamewasili katika mji mkuu wa Saudi, kujadili Syria, huku mataifa yenye nguvu duniani yakishinikiza kuwepo utulivu baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad.
Sweden itachangia meli tatu za kivita katika juhudi za NATO kuongeza uwepo wa muungano huo katika bahari ya Baltic wakati inajaribu kulinda dhidi ya uharibifu wa miundombinu ya chini ya bahari, serikali imesema Jumapili.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, Jumapili ametoa wito kwa washirika wake kuheshimu ahadi zote za kuipatia Ukraine silaha, zikiwemo zile za kukabiliana na mashambulizi ya anga ya Russia.
Nayo wizara ya Ulinzi ya Russia imesema iliingilia kati na iliharibu ndege zisizokuwa na rubani 85 za Ukraine usiku wa kuamkia leo.
Msafara huo ulitoka kutoa pole ya msiba kwa mwenzao ulishambuliwa na majambazi msemaji wa polisi alisema.
Ni baada ya mivutano juu ya mipango ya Addis Ababa kujenga kambi ya jeshi la majini katika mkoa wa Somalia uliojitenga.
Israeli ilithibitisha kwamba mateka aliyekutwa ameuawa huko Gaza alikuwa Hamza Ziyadne, mtoto wa mateka mwingine, Youssef Ziyadne, alikutwa amekufa pamoja naye ndani ya handaki la chini ya ardhi karibu na mji wa kusini wa Rafah.
Jeshi la anga la Ukraine lilisema Ijumaa kuwa Russia iliishambulia kwa ndege 72 zisizo na rubani usiku kucha
Polisi wa Afrika Kusini walisema Ijumaa kuwa wamewaokoa raia 26 wa Ethiopia wasiokuwa na vibali ambao walikuwa wakishikiliwa mateka bila nguo katika nyumba moja mjini Johannesburg
Shirika la misaada ya matibabu- MSF lilisema Ijumaa limelazimika kusimamisha shughuli zake katika mojawapo ya hospitali chache zilizosalia kusini mwa Khartoum kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara
Waziri wa Mambo ya nje wa Italy Antonio Tajani Ijumaa anakwenda Syria kama hatua ya kuunga mkono mpito wa taifa hilo baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu Bashar al-Asaad na wanamgambo wa Kiislamu.
Congo Alhamisi imeipiga marufuku mtandao wa habari wa Al Jazeera kutokana na kutanganza mahojiano yake na kiongozi wa kundi la uasi ambalo limekamata eneo la mashariki mwa nchi katika siku za karibuni.
Pandisha zaidi