Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 17, 2025 Local time: 02:54

Wanamgambo 21 wa serikali wameuawa huko Katsina nchini Nigeria


Maigamji village, Katsina state, Nigeria
Maigamji village, Katsina state, Nigeria

Msafara huo ulitoka kutoa pole ya msiba kwa mwenzao ulishambuliwa na majambazi msemaji wa polisi alisema.

Takriban wanamgambo 21 wa serikali waliuawa katika shambulio la kushtukiza lililofanywa na magenge ya wahalifu katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Katsina, polisi wamesema Ijumaa jioni.

Msafara wa wanamgambo wa serikali waliokuwa wakirejea kutoa rambirambi kwa familia ya mfanyakazi mwenzao aliyekufa ulishambuliwa na majambazi huko Baure, Kijiji kilichopo katika wilaya ya Safana, msemaji wa polisi wa Katsina Abubakar Sadiq Aliyu alisema.

Kwa masikitiko makubwa, watu 21 waliuawa kwa kupigwa risasi kutokana na shambulio hilo, Aliyu alisema, akiongeza polisi wanafanya msako kuhakikisha wahusika wa shambulio lililotokea Jumanne wanakamatwa. Katsina ni moja ya majimbo kadhaa huko kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria yanayotishiwa na majambazi wanaovamia vijiji, kuua na kuwateka wakazi pamoja na kuchoma moto nyumba na kupora mali.

Magenge hayo ambayo yanaweka kambi katika misitu mikubwa kwenye majimbo ya Zamfara, Katsina, Kaduna na Niger, yamejipatia umaarufu kwa utekaji nyara mkubwa wa wanafunzi kutoka mashuleni katika miaka ya hivi karibuni.

Forum

XS
SM
MD
LG