Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 01:23

Wadau wa Syria wakutana kujadili amani


Rais wa zamani wa Syria, aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad
Rais wa zamani wa Syria, aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad

Wanadiplomasia wakuu wa Mashariki ya Kati na Ulaya, Jumapili wamewasili katika mji mkuu wa Saudi, kujadili Syria, huku mataifa yenye nguvu duniani yakishinikiza kuwepo utulivu baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad.

Saudi Arabia, nchi yenye uchumi mkubwa zaidi katika Mashariki ya Kati, inataka kuongeza ushawishi wake Syria baada ya waasi kumuangusha Assad mwezi uliopita, wachambuzi wanasema.

Mazungumzo hayo yatajumuisha mkutano wa maafisa wa Kiarabu pamoja na mkutano unaojumuisha Uturuki, Ufaransa, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa, afisa wa Saudi ameambia AFP.

Kiongozi mpya wa Syria, Ahmed al-Sharaa, ambaye aliongoza kundi kuu la waasi katika muungano uliompindua Assad, anashinikiza kuondolewa vikwazo.

Utawala wake unawakilishwa katika mazungumzo ya Riyadh na Waziri wa Mambo ya Nje, Asaad al-Shaibani. Mataifa ya Magharibi, ikiwemo Marekani na Umoja wa Ulaya, yaliwekea vikwazo serikali ya Assad kutokana na ukandamizaji wake.

Forum

XS
SM
MD
LG