Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 06, 2025 Local time: 20:48

Zelenskiy atoa wito wa kutolewa misaada zaidi kwa nchi yake


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, Jumapili ametoa wito kwa washirika wake kuheshimu ahadi zote za kuipatia Ukraine silaha, zikiwemo zile za kukabiliana na mashambulizi ya anga ya Russia.

Zelenskiy amesema katika wiki iliyopita vikosi vya Russia, vilianzisha mamia ya mashambulizi dhidi ya Ukraine na ambapo takriban mabomu 700 ya anga na zaidi ya ndege 600 zisizo na rubani zilitumika.

Vikosi vya anga vya Ukraine vilitunga ndege 60 kati ya 94 zilizorushwa na Russia, usiku kucha, jeshi la anga limesema Jumapili.

Limesema ndege zisizo na rubani 34 zilipotea, baada ya Ukraine kutumia vifaa vya kueletroniki kubadilisha muelekea wa ndege zisizo na rubani za Russia.

“Kila wiki, vita vya Russia, vinaendelea kwa sababu tu jeshi la Russia, linaendelea kuwa na uwezo wake wa kuitisha Ukraine na kutumia ubora wake angani,” Zelenskiy amesema kwenye mtandao wa Telegram.

Ametoa wito kwa washirika wa Ukraine kutimiza makubaliano ambayo tayari yamefanyika.

Forum

XS
SM
MD
LG