Wizara ya fedha ya Marekani Alhamisi ilitangaza vikwazo dhidi ya Abdel Fattah al-Burhan, ikilituhumu jeshi lake kwa kushambulia shule masoko na hospitali pamoja na kutumia mtindo wa kuwanyima wananchi chakula kama silaha.
Idadi kubwa ya wabunge wanamkata Biden kutoa afueni ili kuzuia mtandao wa TikTok kufungwa nchini Marekani ifikapo Jumapili, na kuonya kuwa mamilioni ya wabunifu na biashara zinaweza kuathiriwa.
Uingereza na Ukraine Alhamisi zilisaini makubaliano ya miaka 100, huku Uingereza ikiahidi kuipa Ukraine msaada wa kijeshi wa dola bilioni 3.6 mwaka huu.
Takriban wanahabari 67 wanafungwa jela barani kote Afrika, hali hiyo ikiashiria changamoto inayoendelea ya kuwa na vyombo vya habari huru, kulingana na ripoti iliyotolewa Alhamisi.
Marekani imemuwekea vikwazo kiongozi wa jeshi la Sudan, ikitaja kuhusika kwake katika uhalifu wa kivita katika mzozo ambao umelitumbukiza taifa hilo lenye utajiri wa mafuta katika hali mbaya tangu mwaka jana, kusababisha njaa, kuua maelfu ya watu na kuwakosesha makazi mamilioni ya wengine.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Alhamisi kwamba mgogoro wa dakika za mwisho na Hamas unazuia idhini ya Israeli ya makubaliano yaliyosubiriwa kwa muda mrefu ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza na kuwaachilia mateka kadhaa.
Waokoaji wa Afrika Kusini walikuwa wakifanya juhudi za mwisho siku ya Alhamisi kufahamu kama kuna mtu yeyote aliyenusurika kwenye machimbo haramu ya dhahabu
Huku muda wa mwisho wa Jumapili ukikaribia kwa Tiktok kutafuta mmiliki mwingine au kukabiliwa na vikwazo vya Marekani, maelfu ya Wamarekani wanaotumia mtandao huo maarufu wa kijamii wanasema wanahamia kwenye program nyingine ya mtandao wa kijamii wa China, Xiaohongshu au RedNote.
Cuba Jumatano ilianza kuwaachia huru wafungwa waliowekwa jela kufuatia maandamano ya kuipinga serikali ya mwaka 2021, kutokana na makubaliano iliyofikia na utawala wa Biden wiki hii.
Rwanda Jumatano ilibadili kauli kufuatia madai yake ya awali kwamba iligundua akiba yake ya kwanza ya mafuta katika Ziwa Kivu, ikisema bado iko kwenye awamu ya uchunguzi na inatafuta washirika.
Israel na Hamas wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano katika awamu kadhaa ambayo yatapelekea kuachiliwa kwa baadhi ya mateka wanaoshikiliwa na kundi hilo la wanamgambo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Wapalestina wana sherehekea makubaliano ya kusitisha mapigano ya Gaza kati ya Israel na Hamas huku WaIsrael wakiwa bado na wasi wasi kuhusu mateka walobaki.
Pandisha zaidi