Waokoaji wa Afrika Kusini walikuwa wakifanya juhudi za mwisho siku ya Alhamisi kufahamu kama kuna mtu yeyote aliyenusurika kwenye machimbo haramu ya dhahabu chini ya ardhi ambapo takriban watu 78 walikufa wakati wakizingirwa na polisi, katika kile chama cha wafanyakazi kiliita mauaji ya kufadhiliwa na serikali.
Polisi walikuwa wameuzingira mgodi huo tangu Agosti na kuzuia chakula na maji kwa wachimbaji hao katika jaribio la kuwalazimisha wachimbaji hao watoke nje ya mgodi ili wakamatwe kama sehemu ya msako dhidi ya uchimbaji haramu wa madini, ambao serikali inauita vita dhidi ya uchumi.
Tangu Jumatatu, waokoaji wametumia ngome ya chuma kutoa maiti 78 na walionusurika 246, baadhi yao wakiwa wamedhoofika na kuchanganyikiwa, katika operesheni iliyoamriwa na mahakama.
Walionusurika ambao wengi wao wanatokea Msumbiji, Zimbabwe na Lesotho wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhamiaji haramu na uchimbaji madini.
Forum