Mahakama ya juu nchini Uganda imeamuru kesi zote zinazowahusu raia katika mahakama ya kijeshi zisitishwe mara moja kusiskilizwa na zihamishwe hadi mahakama za kawaida.
Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda, ambao wanaudhibithi mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamesema wanataka kuendelea kupigana na kuipindua serikali ya Kinshasa.
Waokoaji wanaendelea kutoa mabaki ya ndege mbili zilizogongana angani na kusababisha vifo vya watu 67 karibu na mji mkuu wa Marekani Washington DC, jumatano usiku.
Russia imetekeleza msururu wa mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya Ukraine usiku wa kuamkia leo, na kuwajeruhi watu wanne, kuharibu hospitali na gala ya nafaka katika mkoa wa Odesa.
Jeshi la Israel limesema limepiga ngome za kundi la wanamgambo wa Hezbollah usiku wa kuamkia leo katika bonde la Bekaa, kwenye mpaka wa Syria na Lebanon.
Jeshi la Israel limesema mateka wanane, wakiwemo Waisraeli watatu na raia watano wa Thailand, waliachiliwa Alhamisi huku Israel na Hamas wakifanya ubadilishanaji wa tatu wa mateka na wafungwa chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya zaidi ya miezi 15 huko Gaza.
Kundi la waasi wa M23 Alhamisi limeapa kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, huku wapiganaji wake wakisonga mbele zaidi katika eneo la mashariki mwa nchi lenye utajiri wa madini.
Idara kadhaa za Marekani zimeanzisha uchunguzi kujua chanzo cha kugongana kwa ndege ya abiria ya shirika la American Airlines na helikopta ya jeshi la Marekani karibu na Washington Jumatano usiku.
Wafanyakazi wa huduma za dharura zikiwemo boti na wapiga mbizi walifanya kazi kwenye mto Potomac kuokoa abiria
Ndege ya abiria iligongana na helikopta ya kijeshi ya Marekani Jumatano usiku wakati ilipokuwa inakaribia kutua kwenye uwanja wa ndege wa Washington DC Reagan National, Mamlaka ya usafiri wa anga FAA ilisema.
Jaji Jumatano amemhukumu seneta wa zamani wa Marekani mwenye ushawishi mkubwa kifungo cha miaka 11 jela, baada ya kukutwa na hatia ya rushwa kufuatia kugunduliwa kwa dhahabu nyingi na maelfu ya dola pesa taslimu nyumbani kwake.
Jumuia ya Afrika Mashariki Jumatano imeitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuzungumza na “wadau wote”, wakiwemo wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda, ili kumaliza mapigano katika eneo la mashariki mwa nchi.
Pandisha zaidi