Taarifa ya FAA ilisema ndege ya shirika la American Airlines ilikuwa ikisafiri kutoka Witchita, Kansas, na ilikuwa inakaribia njia yake ya kutua ilipogongana na helikopta aina ya Sikorsky H-60 nyakati za saa tatu usiku.
Hakuna taarifa kuhusu maafa iliyotolewa mara moja.
Maafisa walisema wanajeshi watatu wa Marekani walikuwa ndani ya helikopta hiyo. American Airlines ilisema katika taarifa kwamba abiria 60 na wahudumu wanne walikuwa ndani ya ndege hiyo.
“Tunathibitisha kwamba ndege iliyohusika katika ajali ya usiku ilikuwa helikopta ya kijeshi aina ya UH-60 nje ya Belvoir, Virginia,” jeshi lilisema katika taarifa.
“Tunashirikiana na maafisa wa eneo hilo na tutatoa taarifa pindi zitakapopatikana.”
Shughuli za uokoaji zilianza kwa haraka, ikiwa ni pamoja na boti kwenye Mto Potomac. Ndege huwa zinapita juu ya mto huo kabla ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Reagan National.
Rais wa Marekani Donald Trump alitoa taarifa akisema amefahamishwa kuhusu tukio hilo.
Forum