Israel imesema miongoni mwa sehemu zilizopigwa ni kiwanda cha siri kinachotumika kutengeneza silaha na sehemu nyingine inayohusishwa na uingizaji kwa magendo silaha ndani ya Lebanon.
Israel ilisema jana alhamisi kwamba walinasa ndege isiyokuwa na rubani iliyokuwa inafanya ujasusi kwa msingi kwamba ilikuwa inavunja makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na Lebanon.
Hezbollah na Israel walikubaliana kusitisha vita mwishoni mwa mwezi Novemba na kumaliza mapigano mabaya yaliyoanzia Gaza mwaka 2023.
Marekani ilithibitisha mnamo Jumapili kwamba makubaliano hayo yanayojumulisha siku 60 za wanajeshi wa Israel kuondoka Lebanon, yataendelea kutumika hadi Februari 18.
Israel imetekeleza mashambulizi kadhaa ndani ya Lebanon tangu makubaliano yalipofikiwa, na kuua na kuwajeruhi zaidi ya watu 100.
Forum