Mwanajeshi mwanamke wa Israel Agam Berger aliachiliwa na kukabidhiwa Shirika la Msalaba Mwekundu katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya kaskazini mwa Gaza, na baadaye alikwenda Israel, ambako aliungana tena na wazazi wake.
Saa chache baadaye, msafara wa Shirika la Msalaba Mwekundu ulipita kwenye barabara yenye msongamano iliyojaa umati wa watu katika mji wa kusini mwa Gaza wa Khan Younis ili kuwakabidhi Waisraeli wengine wawili na raia wa Thailand kwa jeshi la Israel.
Jeshi la Israel lilisema Waisraeli hao wataungana na familia zao, huku maafisa wa serikali ya Thailand wakitarajiwa kukutana na raia wao.
Baadaye mchana, kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano, Israel iliwaachilia Wafungwa 110 wa Kipalestina, wakiwemo 32 waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela kutokana na mashambulizi mabaya dhidi ya Waisraeli.
Forum