Hakuna manusura miongoni mwa abiria 64 na wahudumu kwenye ndege ya American Airlines, na watu watatu waliokuwa ndani ya helikopta hiyo aina ya UH-60 Black Hawk, maafisa wa serikali kuu na eneo hilo walisema Alhamisi.
Ndege zote mbili zilianguka ndani ya mto Potomac karibu na uwanja wa ndege wa Reagan National, nje kidogo ya Washington huko Arlington, Virginia.
Shughuli za kutafuta miili zinaendelea.
Waziri wa uchukuzi Sean Duffy, ambaye aliungana na Rais Donald Trump kwenye mkutano na waandishi wa habari huko White House kujadili ajali hiyo, alisema ndege hiyo na helikopta zote zilikuwa na “mifumo ya kawaida ya ndege” iliyosababisha ajali hiyo.
Katika mkutano huo wa waandishi wa habari, Trump aliomba kuwe na dakika moja ya ukimya kuomboleza waathirika na kusema kila mali kwenye ngazi ya serikali za mitaa, majimbo na serikali kuu zitatumiwa kwa ajili ya shughuli za uokoaji na kutafuta miili.
Forum