Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 16:21

M23 wanataka kupindua Felix Tshisekedi


Waasi wa M23 wakiwa wameshika doria mjini Goma
Waasi wa M23 wakiwa wameshika doria mjini Goma

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda, ambao wanaudhibithi mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamesema wanataka kuendelea kupigana na kuipindua serikali ya Kinshasa.

Waasi wamesema hayo wakati rais wa DRC Felix Tshisekedi ametoa wito wa jeshi kuimarishwa, na kuungwa mkono ili kukabiliana na waasi hao, huku Waziri wake wa ulinzi akifutilia mbali uwezekano wa kufanyika mazungumzo.

Waziri wa ulinzi wa DRC Guy Kabombo Muadiamvita, amesema ameelekeza kwamba mipango yoyote ya mazungumzo na waasi wa M23 ifutiliwe mbali mara moja.

Katika ujumbe wa video, Muadiamvita amesema kwamba watapigana kabisa na kama watashindwa, watafia ndani ya Congo.

Waasi wa M23 wameonyesha lengo la kutaka kuongoza mashariki mwa DRC na kusema wapo tayari kwa mazungumzo na serikali ya Tshisekedi.

Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo Rwanda ni mwanachama pia imependekeza mazungumzo.

Forum

XS
SM
MD
LG