Darzeni ya watu wanahofiwa kufariki leo Alhamisi baada ya ndege ya abiria na helikopta ya jeshi la Marekani kugongana wakati ndege hiyo ilipokuwa inakaribia kutua katika uwanja wa ndege wa kitaifa wa Ronald Reagan karibu na Washington.
Wafanyakazi wa huduma za dharura zikiwemo boti na wapiga mbizi walifanya kazi usiku kucha katika maji ya baridi kwenye mto Potomac mkabala na uwanja wa ndege ambako mabaki yalianguka baada ya kugongana takribani saa tatu usiku wa Jumatano.
Maafisa wanasema wanajeshi watatu wa jeshi la Marekani walikuwa kwenye helikopta hiyo wakifanya mafunzo ya uendeshaji ndege. Shirika la ndege la American Airlines ambalo lilifanya safari yake kutoka Wichita, Kansas, hadi Washington limesema katika taarifa kuwa kulikuwa na abiria 60 na wafanyakazi wanne kwenye ndege hiyo.
Maafisa katika mkutano wa mapema Alhamisi na waandishi wa habari hawakuthibitisha vifo vyovyote kutokana na ajali hiyo, wakisema lengo la wakati huo lilikuwa operesheni ya uokoaji.
Forum