Moto mwingine wa nyika umejitokeza na kusambaa kwa kasi katika eneo moja kaskazini mwa Los Angeles Jumatano ukiongezeka kutokana na upepo mkali na hali ya ukavu.
Saratani ya tezi dume ni ugonjwa unaosumbua katika jamii nyingi hivi sasa ugonjwa ambao unaelezwa kwamba unatokana na sababu mbalimbali ikiwemo umri mkubwa au maambukizi ya mara kwa mara katika tezi dume ugonjwa ambao unawakabili wanaume hasa wanaofikia umri mkubwa.
Baraza la Mawaziri la Gabon lilisema Jumatano jioni kwamba uchaguzi wa rais utafanyika Aprili 12, mwaka huu
Waziri wa mambo ya nje wa India Subrah-manyam Jaishankar amesema New Delhi iko tayari kuwapokea raia wa India wasiokuwa na nyaraka halali nchini Marekani
Hata kabla ya kuwepo ofisini kwa saa 48, rais wa Marekani Donald Trump alituma ujumbe wa kukabiliana na China kwenye anga za juu, na kwamba utawala wake utakuwa na ajenda kubwa ifikapo kuendesha Marekani mbele kwenye teknolojia ya akili mnemba au AI pamoja na miundombimu inayoiendesha.
Mamlaka za California Jumatano zimetoa amri ya watu kuondoka kwenye maeneo ya ndani baada ya moto mpya kuzuka ukiwa na upepo mkali kwenye milima iliyopo kasakzini mwa Los Angeles.
Sudan Kusini Jumatano imeamuru kampuni zinazotoa huduma za intaneti kuzuia mitandao ya kijamii, ikiwemo Facebook na TitTok, kufuatia maandamano yenye vurugu yaliyochochewa na vifo vya raia wake wiki iliyopita.
Pentagon itaanza kupeleka hadi wanajeshi 1,500 ili kusaidia kulinda mpaka wa kusini na Mexico katika siku za karibuni.
Polisi wa kundi la Palestina la Hamas walionekana wakishika zamu nje ya jengo la makao makuu yao lililoharibiwa katika mji wa Gaza City Jumatano baada ya makubaliano ya sitisho la mapigano baina ya Hamas na Israel kuanza kutekelezwa.
Maelfu ya watu wameuwawa na wengine zaidi ya milioni 12 wamekoseshwa makazi kutokana na mzozo uliozuka baina ya jeshi la Sudan na kundi la waasi tangu April mwaka 2023.
Nchi tatu zinazotawaliwa na wanajeshi katika kanda ya Sahel zitaungana kuunda kikosi cha wanajeshi 5,000 kupambana na ghasia za wanajihadi ambazo zimekumba mataifa hayo kwa miaka kadhaa, maafisa walisema Jumanne.
Pandisha zaidi