Waziri wa mambo ya nje wa India Subrah-manyam Jaishankar amesema New Delhi iko tayari kuwapokea raia wa India wasiokuwa na nyaraka halali nchini Marekani.
Maoni yake yamekuja kufuatia mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio mjini Washington ambapo uhamiaji haramu ulikuwa mojawapo ya masuala yaliyojadiliwa.
Akisema kwamba New Delhi ilikuwa inapinga vikali uhamiaji haramu, aliwaambia waandishi wa habari kwamba "siku zote tumekuwa tukipokea maoni kama kuna raia wetu ambao hawako hapa kihalali, ikiwa tuna uhakika ni raia wetu, siku zote tuko tayari kwa kurejea kwao India. Alisema ni msimamo ambao India inachukua na kila nchi.
Jaishankar alikuwa akihutubia mkutano wa wanahabari mjini Washington siku ya Jumatano, siku moja baada ya mkutano wake na Rubio.
Forum