Waataalam wa afya wanasisitiza kwamba jamiii isichanganye kati ya ugonjwa wa saratani ya tezi dume, na tezi dume lenyewe, kwasababu tezi dume ni kiungo katika mwili wa mwanaume ambacho kila mwanaume anacho na kazi yake kubwa ni uzalishaji wa mbegu lakini ugonjwa wa tezi dume au saratani ya tezi dume unaanza pale tezi dume linapotanuka.
Daktari Frank Ruta bingwa wa saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini DSM anasema vipimo pekee ndiyo vinaweza kubaini kwanini tezi dume ya mwanaume imetanuka ambapo mgonjwa ataanza kuona dalili mbalimbai ikiwemo kupata haja ndogo mara kwa mara hasa nyakati za usiku.
Je ni kweli saratani ya tezi dume haina matibabu ya mgonjwa kupona kabisa ? Daktari Frank Ruta bingwa wa saratani anabainisha kwamba kuna dhana potofu kuwa matibabu ya saratani yanaua mgonjwa lakini anasema, muhimu ni mgonjwa kupata matibabu mapema, kabla ugonjwa huo haujasambaa. Hivyo basi ameshauri jamii ambayo ni wanaume kuwa na utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara kwasababu pia dalili za ugonjwa huu hazionekana kwa urahisi.
Kuna ambao wanasumbuliwa na ugonjwa huu wa saratani ya tezi dume na kwa imani hizo hizo kwamba hospitalini hakuna tiba ya uhakika ya kupona, hawa wanakimbilia kwenye wataalam wa tiba mbadala.
Tumezungumza na Tabibu Maduhu kutoka Taasisi ya tiba mbadala ya Yasosi Traditional Medicine Magomeni jijini DSM yeye licha ya kudai kwamba ana dawa za tiba asili za maradhi hayo mbazo anaema zimethibitishwa na wizara ya afya , anashauri hata hivyo jamii hasa wanaougua magonjwa sugu kuacha tabia ya kukimbilia tiba mbadala bila kuwa na uhakika na ubora wake.
Forum