Israeli ilithibitisha kwamba mateka aliyekutwa ameuawa huko Gaza alikuwa Hamza Ziyadne, mtoto wa mateka mwingine, Youssef Ziyadne, alikutwa amekufa pamoja naye ndani ya handaki la chini ya ardhi karibu na mji wa kusini wa Rafah.
Jeshi la anga la Ukraine lilisema Ijumaa kuwa Russia iliishambulia kwa ndege 72 zisizo na rubani usiku kucha
Polisi wa Afrika Kusini walisema Ijumaa kuwa wamewaokoa raia 26 wa Ethiopia wasiokuwa na vibali ambao walikuwa wakishikiliwa mateka bila nguo katika nyumba moja mjini Johannesburg
Shirika la misaada ya matibabu- MSF lilisema Ijumaa limelazimika kusimamisha shughuli zake katika mojawapo ya hospitali chache zilizosalia kusini mwa Khartoum kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara
Waziri wa Mambo ya nje wa Italy Antonio Tajani Ijumaa anakwenda Syria kama hatua ya kuunga mkono mpito wa taifa hilo baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu Bashar al-Asaad na wanamgambo wa Kiislamu.
Congo Alhamisi imeipiga marufuku mtandao wa habari wa Al Jazeera kutokana na kutanganza mahojiano yake na kiongozi wa kundi la uasi ambalo limekamata eneo la mashariki mwa nchi katika siku za karibuni.
Russia imesema Alhamisi kwamba inafuatilia kwa karibu hali ya huko Greenland, baada ya rais mteule wa Marekani Donald Trump kukatata kufuta uwezekano wa kutumia jeshi na hatua za kiuchumi kuchukua udhibiti wa eneo hilo kutoka Denmark.
Mondlane alidai kwamba ameshinda uchaguzi wa Oktoba mwaka jana uliokuwa na ushindani mkali nchini Msumbiji
Watanzania wametakiwa kusimama pamoja na kupaza sauti dhidi ya vitendo vya utekaji vinavyoendelea nchini na jeshi la polisi latakiwa kukubali uwepo wa vitendo hivyo na kuwajibika kwa kufanya uchunguzi
Rais Joe Biden Jumatano ameidhinisha tangazo la msaada wa dharura wa serikali kuu kwa ajili ya mioto ya msituni ya California, utakao fadhili utoaji wa fedha na rasilimali nyingine za kupambana na janga hilo.
Maelfu ya watu Jumatano walikumbana na baridi kali ili kwenda katika jengo la Bunge la Marekani, ili kutoa heshima zao za mwisho kwa rais wa zamani Jimmy Carter, amabye mwili wake umelazwa katika jengo hilo kabla ya mazishi yake ya kiserikali ya kifahari kufanyika Alhamisi.
Watu wenye silaha Jumatano waliishambulia Ikulu ya Chad katika mji mkuu N’Djamena, na kuzua mapigano ambayo yaliua washambuliaji 18 na afisa mmoja wa usalama na wengine kadhaa kujeruhiwa, serikali ilisema.
Pandisha zaidi