Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 10, 2025 Local time: 11:44

Maelfu wakusanyika Washington Jumatano ili kutoa heshima za mwisho kwa Jimmy Carter


Jeneza la Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter kwenye majengo ya bunge la Marekani Jumatano.
Jeneza la Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter kwenye majengo ya bunge la Marekani Jumatano.

Maelfu ya watu Jumatano walikumbana na  baridi kali ili kwenda katika jengo la Bunge  la Marekani, ili kutoa heshima zao za mwisho kwa  rais wa zamani Jimmy Carter, amabye mwili wake umelazwa  katika jengo hilo kabla ya mazishi yake ya kiserikali  ya kifahari kufanyika Alhamisi.

Waombolezaji ambao walijumuisha maafisa kadhaa waliochaguliwa pamoja na makamu wa rais Kamala Harris, waliangazia baadhi ya mafanikio yake na ubinadamu wa kiongozi huyo aliyefariki mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 100.

David Smith profesa kwenye chuo cha Carter cha Amani na Usuluhishi wa Mizozo kwenye chuo kikuu cha George Mason, alisema kuwa rais huyo wa zamani alikuwa na ushawishi mkubwa kwenye maisha yake, wakati akiambia VOA kwamba alifika Bungeni, ili kutoa heshima zake mwisho kwa Carter pamoja na miradi aliyobuni.

Forum

XS
SM
MD
LG