Kiongozi wa upinzani nchini Msumbiji Venancio Mondlane amerejea kutoka uhamishoni leo Alhamisi, akidai kuwa ameshinda uchaguzi wa Oktoba uliokuwa na ushindani mkali, lakini vikosi vya usalama baadaye vilitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wake waliokusanyika kumsalimia.
Upigaji kura wa Oktoba 9 mwaka jana uliokuwa na utata, ambao Mondlane anasema kura ziliibiwa, umezusha maandamano katika miezi michache iliyopita ambapo mamia ya waandamanaji wameuawa katika taifa hilo la kusini mwa Afrika lenye watu milioni 35.
Kurejea kwangu hakujatokana na makubaliano yoyote ya kisiasa. Kurejea kwangu ni uamuzi wa upande mmoja wa kurudi nchini Msumbiji, aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Maputo wakati alipowasili.
Niko hapa kuthibitisha kwamba sikuondoka Msumbiji kwa hofu, alisema, akimaliza kipindi cha uhamishoni ambacho kilianza siku chache baada ya upigaji kura, wakati Mondlane aliposema maisha yake yalikuwa hatarini.
Forum