Jeshi la anga la Ukraine lilisema Ijumaa kuwa Russia iliishambulia kwa ndege 72 zisizo na rubani usiku kucha ingawa iliangusha ndege 33 huku nyingine 34 zilitoweka kwenye rada bila kufikia malengo yao.
Ndege tano zisizo na rubani zilishambulia majengo mbalimbali katika eneo la kaskazini mwa mkoa wa Chernihiv, na kumjeruhi mtu mmoja, jeshi la anga lilisema.
Ndege isiyo na rubani iliangukia kwenye jengo katika mji mkuu wa Kyiv lakini haikusababisha majeruhi.
Picha za video zilizorekodiwa na Reuters zilionyesha
mlipuko na moto unaowaka kwa mbali huko Kyiv
wakati wa shambulio la usiku.
Forum