Hata hivyo rais ametahadharisha kuwa mchakato huo utachukua muda. Idara ya zima moto ya Kaunti ya Los Angeles imekumbana na mioto minne hatari kwa maisha, ambayo imeuwa watu wawili na kuchoma zaidi ya majengo 1,000, na kuwalazimisha maelfu ya watu kuondoka makwao.
Mkuu wa idara zima moto ya kaunti ya LA, Anthony C. Marrone, amesema Jumatano kwamba Idara yake ilijitayarisha kukabiliana na mioto miwili ya msituni na wala siyo minne, iliyosabaishwa na upepo mkali pamoja na uhaba wa unyevu nyevu hewani. Amesema kuwa zaidi ya hektari 2,000 zimeungua, wakati moto ukiendelea kusambaa.
“Hatuna uwezo wa kuudhibiti,” amesema Marrone. Maafisa wa kieneo wamewataka wakazi kuhakikisha wanafuata maagizo ya kwenda maeneo usalama. Walinzi wa Kitaifa 2,000 tayari wamepelekwa ili kuwasaidia zima moto wa huko. Jumatano jioni, ndege ya kusaidia kuzima moto ilisimamisha shughuli zake kwasababu ya upepo mkali wakati ilipokuwa hewani ikidondosha maji na kujaribu kuzima moto.
Forum