Serekali ya Pakistani, Jumamosi imesema kwamba wanajeshi wasiopungua 18 wameuwawa katika shambulizi la usiku wa kuamkia jana katika jimbo la Balochistan, likiashiria moja ya siku mbaya zaidi kwa vikosi vya usalama katika miezi ya hivi karibuni.
Hamas iliwakabidhi mateka watatu wa Israel, Jumamosi, ikiwa ni mfululizo wa mabadilishano ya karibuni katika makubaliano yenye lengo la kumaliza mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Palestina.
Mashambulizi ya wanamgambo wa Sudan, yameuwa watu 54 katika soko la mji mkuu pacha wa Omdurman, Jumamosi kwa mujibu wa chanzo cha madakatari kilichozungumza na shirika la habari la AFP.
Russia, Jumamosi imesema imekikamata kijiji kilichoko mashariki mwa mji wa Toretsk, nchini Ukraine, huku Kyiv ikisema kuwa watu wanne wameuawa katika mashambulizi ya usiku ya Russia.
Mahakama ya juu nchini Uganda imeamuru kesi zote zinazowahusu raia katika mahakama ya kijeshi zisitishwe mara moja kusiskilizwa na zihamishwe hadi mahakama za kawaida.
Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda, ambao wanaudhibithi mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamesema wanataka kuendelea kupigana na kuipindua serikali ya Kinshasa.
Waokoaji wanaendelea kutoa mabaki ya ndege mbili zilizogongana angani na kusababisha vifo vya watu 67 karibu na mji mkuu wa Marekani Washington DC, jumatano usiku.
Russia imetekeleza msururu wa mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya Ukraine usiku wa kuamkia leo, na kuwajeruhi watu wanne, kuharibu hospitali na gala ya nafaka katika mkoa wa Odesa.
Jeshi la Israel limesema limepiga ngome za kundi la wanamgambo wa Hezbollah usiku wa kuamkia leo katika bonde la Bekaa, kwenye mpaka wa Syria na Lebanon.
Jeshi la Israel limesema mateka wanane, wakiwemo Waisraeli watatu na raia watano wa Thailand, waliachiliwa Alhamisi huku Israel na Hamas wakifanya ubadilishanaji wa tatu wa mateka na wafungwa chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya zaidi ya miezi 15 huko Gaza.
Kundi la waasi wa M23 Alhamisi limeapa kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, huku wapiganaji wake wakisonga mbele zaidi katika eneo la mashariki mwa nchi lenye utajiri wa madini.
Idara kadhaa za Marekani zimeanzisha uchunguzi kujua chanzo cha kugongana kwa ndege ya abiria ya shirika la American Airlines na helikopta ya jeshi la Marekani karibu na Washington Jumatano usiku.
Pandisha zaidi