Waumini wamekusanyika huko Saint Peters Square na nje ya hospitali ya Gemelli siku ya Jumanne wakati Papa Francis akiwa bado katika hali mahututi.
Ugonjwa usiojulukana umeuwa watu zaidi ya 50 huko kaskazini magharibi mwa Congo, kulingana na madaktari wa eneo hilo na shirika la Afya Duniani siku ya Jumatatu.
Uingereza Jumanne ilisema itasitisha msaada wa nchi kwa nchi kwa Rwanda na kuweka vikwazo vingine vya kidiplomasia kwa Kigali kutokana na jukumu lake katika mzozo katika nchi jirani ya Kongo.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alisema kwamba “zaidi ya watu 7,000” wameuawa mashariki mwa nchi tangu mwezi Januari, wakati waasi ambao inasemekana wanaungwa mkono na Rwanda walipoteka miji miwili mikubwa.
Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatatu alisema kwamba nchi yake haipingi kushirikishwa kwa Ulaya katika mazungumzo ya amani kati ya Russia na Marekani yenye lengo la kumaliza vita vya Ukraine.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu lilipitisha azimio lilioandikwa na Marekani siku ya kumbukumbu ya miaka mitatu ya uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine, azimio ambalo linachukua msimamo wa kutoegemea upande wowote katika mzozo huo.
Mazungumzo hayo ni ya kwanza kutangazwa hadharani kati ya waasi na mamlaka ya Senegal iliyochaguliwa mwezi Machi mwaka jana
Viongozi hao walifanya mazungumzo wakati Rais wa Marekani Donald Trump akishinikiza kufikiwa makubaliano ya kumaliza vita vya Ukraine
Mazungumzo na Israel kupitia wapatanishi kuhusu hatua zijazo katika makubaliano ya kusitisha mapigano yana masharti ya kuwaachilia wafungwa wa Kipalestina kama ilivyokubaliwa, afisa wa Hamas Basem Naim alisema Jumapili.
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Jumapili alisema uongozi mbaya wa mrithi wake, Rais Felix Tshisekedi umechangia pakubwa kwa kuzidisha mzozo mashariki mwa nchi.
Marekani na Ukraine Jumapili zimesema zinakaribia kufikia makubaliano kwa Kyiv Kuipa Washington Sehemu kubwa ya madini yake nadra kama malipo ya fidia kwa mabilioni ya dola ya zana za kijeshi ambazo Marekani iliipa Ukraine kujihami dhidi ya vita vya Russia.
Waconservative nchini Ujerumani wameshinda uchaguzi wa taifa Jumapili lakini uchaguzi huo wenye kura zilizosambaratika umekipa chama cha mrengo mkali wa kulia cha Alternative for Germany (ADF) matokeo yake mazuri kwa kupata nafasi ya pili.
Pandisha zaidi