Papa amekutana na viongozi wenzake wakuu akiwa hospitali kujadili masuala ya kazi, Vatican imesema siku ya Jumanne, na maafisa wamesema alikuwa akila kama kawaida na anatembea.
Papa mwenye umri wa miaka 88 amekuwa katika hopitali ya Rome ya Gemelli kwa siku ya 12, muda mrefu kwa papa kulazwa hospitali katika miaka yake 12 ya upapa.
Afisa wa Vatican, ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu hakuwa na mamlaka ya kujadili hali ya papa, amesema Francis anakula kama kawaida, anatembea katika chumba chake cha hospital, na anaendelea na matibabu.
Vatican imesema Francis amekutana na kadinali Pietro Parolin wa pili anayemfuatia katika safu yake na naibu wa Parolin siku ya Jumatatu.
Forum