Taarifa fupi ya mapema Jumapili haikutaja endapo Papa Francis alitoka kitandani au kupata kifungua kinywa, kama alivyofanya siku zilizopita.
Taarifa ilieleza kuwa usiku ulipita vyema, na Papa alipumzika.
Vaticani baadaye ilisema PapaFrancis alikuwa na fahamu, akiendelea kupokea oksijeni ya ziada na kwamba uchunguzi zaidi wa kliniki ulikuwa ukifanywa. Taarifa za kina zaidi za matibabu zilitarajiwa kutolewa baadaye Jumapili.
Siku ya Jumamosi, madaktari walisema Papa huyo mwenye umri wa miaka 88, ambaye sehemu ya pafu moja ilitolewa akiwa kijana, alikuwa katika hali mbaya baada ya kukumbwa na tatizo la muda mrefu la ugonjwa wa pumu alipotibiwa Nyumonia na maambukizi tata ya mapafu.
Forum