Hamas imewaachilia huru mateka wengine watatu wa Israel, Jumamosi kama sehemu ya makubaliano tete ya kusitisha mapigano, hata wakati Rais wa Marekani, Donald Trump, anaendelea kuendeleza mpango wake wa kumiliki Ukanda wa Gaza.
Afrika Kusini, Jumamosi imekosoa uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump, kusimamisha msaada kwa nchi hiyo kutokana na sheria aliyodai inaruhusu ardhi kunyakuliwa kutoka kwa wakulima wa kizungu.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, na mwenzake wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, walishiriki mkutano wa Jumamosi, Tanzania, ambapo viongozi wa kikanda walitoa mwito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano nchini DRC.
Rwanda ilisema Ijumaa kwamba ina ushahidi wa mpango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufanya shambulizi dhidi yake, na kukanusha kuwa ilikuwa ikichochea migogoro ndani ya mpaka wa nchi hiyo, jirani yake.
Utawala wa Trump umewasilisha mpango wa kupunguza wafanyakazi ulimwenguni kote, kwenye miradi inayopokea misaada kutoka Marekani, kama sehemu ya kulivunja shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani, USAID, na kusalia na takriban wafanyakazi 300.
Zaidi ya maafisa wa polisi 100 wa Kenya waliwasili katika mji mkuu wa Haiti Alhamisi kuimarisha juhudi za kurejesha usalama za kikosi cha kimataifa ambacho mustakabali wake unatishiwa na hatua ya Marekani ya kusitisha sehemu ya ufadhili wake kwa kikosi hicho.
Ikulu ya Marekani imesema Alhamisi kwamba inafanya tathmini ya kina ya malalamishi yaliyowasilishwa na China kwa Shirika la Kimataifa la Biashara, WTO.
Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Afya Duniani WHO, huko Gaza amesema Alhamisi kuwa njia zaidi za kutoka zinahitajika ili kufanya uokozi wa kimatibabu kwa maelfu ya Wapalestina wakiwemo watoto ambao wanahitaji missada ya kuokoa maisha.
Marekani ina jukumu la kimkataba la kulinda mfereji wa Panama endapo utashambuliwa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesema Alhamisi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio Jumatano ametangaza kwamba Marekani inapanga kuunga mkono Guatemala na miradi mipya ya miundombinu pamoja na kuondolewa ushuru kwenye misaada ya kigeni ili kuimarisha ushirika wa Marekani na taifa hilo la Amerika ya Kati.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia wakimbizi na uhamiaji kwa pamoja Jumatano yameelezea wasi wasi wao kuhusu mpango wa Pakistan wa kuanza mchakato mpya wa kurejesha halaiki ya wahamiaji wa Afghanistan pamoja na waomba hifadhi.
Karibu watu 70 wameuwawa na wengine 50 kujeruhiwa kufuatia mapigano ya saa 24 kati ya wapiganaji wa Islamic State na vikosi vya eneo la Somalia la Puntland.
Pandisha zaidi