Wanamgambo wa Sudan wamewaua zaidi ya watu 200 wakiwemo wanawake na watoto, katika shambulio la siku tatu kwenye vijiji vya kusini mwa nchi hiyo, kundi la wanasheria linalofuatilia vita nchini humo lilisema Jumanne.
Ghasia kati ya makundi hasimu ya magenge zimeua watu 14 mwishoni mwa wiki kwenye mji wa bandari wa Equador wa Guayaquil ambao ni kitovu cha mivutano kati ya magenge, polisi wamesema Jumatatu.
Utalawa wa Trump umeanza kufuta kazi mamia ya wafanyakazi wa idara ya safari za anga na kusababisha hali ya sintofahamu kuelekea kwa wikiendi yenye shughuli nyingi za usafiri wa anga, wiki chache baada ya ajali mbaya ya ndege mbili karibu na uwanja wa ndege wa Reagan mjini Washington DC.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio Jumatatu akiwa Saudi Arabia amefanya mazungumzo kuhusu sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas pamoja na hatma ya Gaza baada ya hali ya utulivu kurejea.
Watu 20 waliuawa Jumatatu kaskazini mwa Mali wakati magari waliyokuwa wakisafiria yaliposhambuliwa, huku vyanzo vya eneo hilo vikiiambia AFP kwamba mamluki wa Wagner na jeshi la Mali walihusika katika mauaji hayo.
Kenya imetangaza kuwa inahitaji bilioni 24.9 kukidhi huduma za afya baada ya Marekani kusitisha misaada
Rubio yupo Saudi Arabia huku kukiwa na upinzani kuhusu pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwaondoa Wapalestina kutoka Gaza
Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika siku za hivi karibuni wameahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza.
Walioshuhudia tukio waliliambia shirika hilo la habari la serikali kuwa mlipuko wa mitungi ya gesi ulisababisha kuanguka kwa jengo hilo
Serikali ya Uganda Jumapili ilisema itaiondoa kesi dhidi ya mpinzani mkongwe Kizza Besigye katika mahakama ya kijeshi, na kumtaka asitishe mgomo wa kula gerezani, waziri mmoja amesema.
Nyota wa muziki, raia wa Colombia Shakira, Jumapili amelazimika kusitisha show yake huko Lima, Peru, na baadaye kupelekwa hospitalini kutokana na maumivu ya tumbo.
Pandisha zaidi