Jengo moja lililoanguka katika mji mkuu wa Misri liliua watu 10 na kuwajeruhi wengine wanane leo Jumatatu, huku wengine kadhaa wakiaminika kufukiwa chini ya vifusi, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Magari ya kubeba wagonjwa yalipelekwa kwenye eneo la tukio katika makazi ya watu wa daraja la wafanyakazi huko Kerdasa, ambako timu za ulinzi wa raia ziliwatafuta watu wanaodhaniwa wamefunikwa chini ya vifusi, kulingana na gazeti la Al-Akhbar Al-Youm.
Walioshuhudia tukio hilo waliliambia shirika hilo la habari la serikali kwamba mlipuko wa mitungi ya gesi ulisababisha kuanguka kwa jengo hilo na uchunguzi wa polisi unaendelea. Kanuni za ujenzi zinatekelezwa bila usawa katika mji mkuu wa Cairo, makazi ya watu zaidi ya milioni 26.
Mji huo umeshuhudia vifo kutokana na kuanguka kwa majengo kadhaa katika miaka ya hivi karibuni kwa sababu ya hali dhaifu kwa baadhi ya majengo na wakati mwingine kushindwa kuzingatia kanuni za ujenzi.
Forum