Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 23:45

Zaidi ya raia 200 wameuwa na wanamgambo wa Sudan wiki hii - Ripoti


Wapiganaji wa Sudan.
Wapiganaji wa Sudan.

Wanamgambo wa Sudan wamewaua zaidi ya watu 200 wakiwemo wanawake na watoto, katika shambulio la siku tatu kwenye vijiji vya kusini mwa nchi hiyo, kundi la wanasheria linalofuatilia vita nchini humo lilisema Jumanne.

Kikosi cha wanamgambo cha RSF, kilicho katika vita vya takriban miaka miwili na jeshi la kawaida la Sudan, "kilivamia raia wasio na silaha katika maeneo ambayo hayana wanajeshi" katika vijiji vya Al-Kadaris na Al-Khelwat, katika jimbo la White Nile, kulingana na kundi la Wanasheria linalofuatilia visa vya ukiukaji wa haki.

Kundi hilo liliongeza kuwa RSF ilifanya "mauaji, utekaji nyara, kulazimisha watu kutoroka, na uporaji wa mali" wakati wa shambulio hilo lililoanza siku ya Jumamosi, ambalo pia limeacha mamia wakiwa wajeruhiwa na wengine kutoweka.

Kulingana na kundi hilo, baadhi ya wakazi walipigwa risasi walipokuwa wakijaribu kutoroka kuvuka Mto Nile. Baadhi wamekufa maji kutokana na hilo, mawakili hao walisema, wakitaja shambulio hilo dhidi ya wanakijiji kuwa ni "mauaji ya kimbari".

Tangu Aprili 2023, Sudan imekumbwa na mzozo wa kikatili uliosababishwa na uhasama kati ya vikosi vya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani, kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Daglo.

Forum

XS
SM
MD
LG