Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 22:56

Mamia ya wafanyakazi wa safari za ndege Marekani wapoteza ajira


Picha ya ndege aina ya Boeing 737 Max .
Picha ya ndege aina ya Boeing 737 Max .

Utalawa wa Trump umeanza kufuta kazi mamia ya wafanyakazi wa idara ya safari za anga na kusababisha hali ya sintofahamu kuelekea kwa wikiendi yenye shughuli nyingi za usafiri wa anga, wiki chache baada ya ajali mbaya ya ndege mbili karibu na uwanja wa ndege wa Reagan mjini Washington DC.

Wafanyakazi waliokuwa wameajiriwa hivi karibuni walikuwa wa kwanza kupata barua pepe Ijumaa wakielezwa kuwa wamefutwa. Hayo ni kwa mujibu wa mkuu wa shirikisho la Usalama wa Safari za Ndege David Spero.

Miongoni mwa wafanyakazi waliyoathiriwa ni pamoja na wasimamizi wa mitambo wa FAA, wasimamizi wa kuruka na kupaa kwa ndege kulingana na taarifa ya mmoja wa wafanyakazi ambaye hakutaka kutajwa kwa kuwa hajaruhusiwa kuongea na vyombo vya habari.

Shirikisho la waratibu wa safari za ndege limesema Jumatatu kwamba linatathmini athari za usalama wa safari za ndege kufuatia kufutwa kwa wafanyakazi hao. Taarifa zimeongeza kuwa wafanyakazi hao wanafutwa wakati tayari kukikuwa na upungufu wa wafanyakazi waliokuwa wakilalamikia kodi za juu na upungufu wa wafanyakazi, pamoja na wasi wasi wa usalama wa safari za ndege.

Forum

XS
SM
MD
LG