Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kuwa mwenyeji wa kundi la viongozi wa Ulaya kwa ajili ya mazungumzo leo Jumatatu yanayolenga hali nchini Ukraine huku kukiwa na mabadiliko katika mwelekeo wa Marekani kuhusu mzozo na mapendekezo ya maafisa wa Marekani kwamba Ulaya haitakuwa na jukumu katika mazungumzo ya amani.
Miongoni mwa wale wanaotarajiwa kuhudhuria ni viongozi kutoka Uingereza, Ujerumani, Italia, Poland, Uhispania, Uholanzi na Denmark. Mkuu wa NATO, Mark Rutte, Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa, na Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen pia walitarajiwa kushiriki.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika siku za hivi karibuni wameahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer akisema serikali yake iko tayari kutuma wanajeshi wake nchini Ukraine kama sehemu ya kikosi chochote cha kulinda amani baada ya vita.
Forum