Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 03, 2025 Local time: 04:02

Rubio afanya mazungumzo ya sitisho la mapigano la Gaza akiwa Saudi Arabia


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio akiwa na mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman Jumatatu. Feb 17, 2025.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio akiwa na mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman Jumatatu. Feb 17, 2025.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio Jumatatu akiwa Saudi Arabia amefanya mazungumzo kuhusu sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas pamoja na hatma ya Gaza baada ya hali ya utulivu kurejea.

Rubio alikutana na mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman, na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Faisal bin Farhan. Mazungumzo hayo yamefanyika siku chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa Wapalestina milioni 2.3 wanahitaji kuondolewa Gaza na kupelekwa kwenye mataifa jirani na kisha Marekani kukarabati eneo hilo lililopo karibu na bahari ya Mediterranean, wazo ambalo linapingwa vikali na Saudi Arabia pamoja na mataifa mengine ya kiarabu.

Rubio na mwanamfalme Mohammed bin Salman walizungumzia umuhimu wa usalama wa Gaza kwa ajili ya usalama wa kieneo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Tammy Bruce amesema kuwa maafisa hao walizungumzia umuhimu wa kutekelezwa kwa sitisho la mapigano la Gaza. Mataifa ya Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia yanaendelea kuunga mkono kuundwa kwa taifa huru la Palestina litakalojumuisha Gaza, kupakana na Israel. Kwa muda mrefu huo ndio umekuwa msimamo wa Marekani, lakini utata umezuka katika siku za karibuni kufuatia madai ya Marekani kwamba ingependa kumiliki Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG