China imesema kwamba ipo tayari kushirikiana na Umoja wa Ulaya kukabiliana na changamoto zinazoukumba ulimwengu.
Serikali ya muungano wa kitaifa ya Afrika Kusini inayumba yumba kutokana na tofauti kati ya vyama tanzu vinavyounda serikali, lakini rais Cyril Ramaphosa amesema serikali hiyo ni thabithi.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka Marekani kuchukua umiliki wa Gaza, hatua inayovuka matamshi yake ya kuwalazimisha wapalestina kuondoka katika eneo eneo lililokumbwa na mapigano na kuhamia nchi jirani za Jordan na Misri.
Marekani imeufahamisha rasmi Umoja wa Mataifa kwamba imesitisha ufadhili wake kwa kikosi kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambacho kilikuwa na jukumu la kupambana na magenge yanayojaribu kudhibiti mji mkuu wa Haiti, Umoja wa Mataifa ulisema Jumanne.
Takriban watu 10 Jumanne wameuwawa kwenye ufyatulianaji wa risasi kwenye kituo kimoja cha elimu kati kati mwa Sweden akiwemo mshambuliaji, maafisa wa polisi wamesema.
Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kusisitiza mpango wake wa kuondolewa kwa Wapalestina kutoka Gaza wakati akiwa mwenyeji wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu huko White House Jumanne.
Wachambuzi wa mambo wanasema kwamba Kundi la wanamgambo la Sudan -RSF limeanza kupoteza nguvu dhidi ya jeshi la taifa kutokana na makosa ya mikakati, ugomvi wa ndani kati ya viongozi wake na kupungua vifaa.
Rubio alikuwa nchini El Salvador kwa mazungumzo na Rais Nayib Bukele na alitangaza kuwa Bukele alikubali kupokea wahamiaji kutoka Marekani
Maafisa wa huduma za dharura wa Israel wamesema watu wasiopungua sita wamejeruhiwa wakiwemo wanajeshi wawili.
Wakati huo huo jeshi la Ukraine limesema ulinzi wake wa angani ulitungua ndege 37 kati ya 65 zisizokuwa na rubani za Russia.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumatatu amesitisha kwa muda ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa kutoka Mexico na Canada zinazoingia hapa Marekani kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuzungumza na rais wa Mexico Claudia Sheinbaum na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.
Mapigano makali huko kusini na magharibi mwa Sudan yaliua watu 65 na kujeruhi wengine zaidi ya 130 Jumatatu, madaktari wamesema, huku vita vibaya kati ta jeshi na kundi la wanamgambo vikipamba moto tena.
Pandisha zaidi