“Nafikiri wanahitaji kupewa ardhi mpya inayopendeza na tutafute watu kadhaa watakao itengeneza na kuifanya inayoweza kukalika,” Trump aliambia wanahabari kabla ya kushiriki kikao na Netanyahu.
Tangazo hilo lilifuatia pendekezo la kushtukiza la Trump mapema Jumanne la kuhamishwa kwa kudumu kwa Wapalestina kutoka Gaza hadi kwenye nchi jirani.
Akizungumza na wanahabari awali kwenye White House, mjumbe wa Marekani huko Mashariki ya Kati Steve Witkoff aliashiria kuwa utawala wa Trump unatathmini mashauriano zaidi kuhusu mkataba wa sitisho la mapigano uliotangazwa Januari 19, siku moja kabla ya kuapishwa kwa Trump.
Mwezi uliopita, Trump alipendekeza kuwa angependa Jordan na Misri wapokee Wapalestina zaidi kama sehemu ya juhudi za kusafisha Gaza.
Forum