Wizara ya mambo ya nje ya China imesema hayo wakati Umoja wa Ulaya unajitayarisha na uwezekano wa kuwekewa nyongeza ya ushuru kutoka Marekani.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian, amesema kwamba China inatambua umuhimu mkubwa wa ushirikiano na Umoja wa Ulaya na kwamba ina matumaini ushirikiano huo utakuwa wa kutegemewa.
Mkuu wa biashara wa Umoja wa Ulaya amesema kwamba umoja huo unataka kujadiliana kwa haraka sana na Marekani kuhusu mpango wa Donald Trump kuiwekea vikwazo.
Rais wa tume ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen ametabiri kwamba mazungumzo na Washington yatakuwa magumu.
Forum