Australia imeahidi kuendelea kutoa msaada mkubwa kwa nchi za kusini mwa Pacific, katika mkutano kuhusu usalama na Uchumi, uliofanyika leo Alhamisi na Vanuatu wakati wa thathmini ya athari zinazoweza kutokea kufuatia hatua ya rais Donald Trump kupunguza msaada wa Marekani nje ya nchi.
Wanadiplomasia wa Marekani na Russia wamekutana leo alhamisi Istanbul kwa mazungumzo kuhusu utendakazi wa balozi zao mjini Moscow na Washington.
Vatican imesema kwamba kiongozi wa kanisa la katoliki Papa Francis, amelala vyema usiku wa kuamkia leo na kwamba alikuwa anapumzika, akiwa bado hospitalini mjini Rome ambapo anatibiwa homa ya mapafu.
Marekani itawekeza hadi dola bilioni 1 kukabiliana na kusambaa kwa mafua ya ndege, pamoja na kuongeza uagizaji wa mayai kutoka nje katika juhudi za kupunguza bei ghali ya bidhaa hiyo, waziri wa kilimo Brooke Rollins alisema Jumatano.
Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco Jumatano aliwataka raia wa nchi hiyo kutofanya ibada ya kuchinja kondoo wakati wa siku kuu ya Eid al-Adha mwaka huu kutokana na kupungua kwa mifugo nchini humo kufuatia ukame wa miaka mingi.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai Jumatano alisema mahakama za kimataifa zimeshindwa kukomesha ukatili wa miongo mitatu katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumatano alisema kwamba yeye na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy wataisini mkataba unaoipa Marekani haki ya kupata madini adimu ya Kyiv yenye faida kubwa.
Serikali ya Uganda imesema Jumatano kwamba mmoja wa wake na watoto watatu wa kiongozi wa uasi kutoka Uganda Joseph Kony wamerejeshwa Uganda kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Serikali kuu ya Somalia na Umoja wa Afrika wamekubaliana kuhusu idadi ya wanajeshi kutoka nchi mbalimbali watakaohudumu katika kikosi kipya cha Umoja wa Afrika kufuatia wiki kadhaa za mtafaruku kati ya Ethiopia na Somalia na pia kati ya Somalia na Burundi.
Zaidi ya wanamgambo 70 wa kundi la Al-Shabaab waliuawa nchini Somalia katika operesheni ya jeshi kwa ushirikiano na vikosi vya ndani, wizara ya habari ilisema Jumanne.
Wahamiaji zaidi wanaotarajiwa kufukuzwa kutoka nchini Marekani waliwasili katika kituo cha kuwashikilia kwa muda cha Guantanamo Bay, nchini Cuba.
Waumini wamekusanyika huko Saint Peters Square na nje ya hospitali ya Gemelli siku ya Jumanne wakati Papa Francis akiwa bado katika hali mahututi.
Pandisha zaidi