Kyiv itailipa fidia Washington kwa silaha ilizoipa Ukraine kupambana katika vita vya miaka mitatu vya uvamizi wa Russia.
Akiongoza mkutano wa kwanza wa baraza lake la mawaziri katika muhula wake mpya, Trump alisema Zelenskiy atakuwa White House Ijumaa kusaini mkataba huo na kwa ajili ya majadiliano kuhusu hali ya vita.
Trump alisema mkataba huo “unatuletea utajiri mkubwa”, lakini alisema lengo lake kuu ni kumaliza vita, ambavyo vimeua maelfu ya watu au kujeruhi maelfu kadhaa ya wanajeshi wa Russia na Ukraine na raia wa Ukraine.
“Lengo langu la pili, ni kupokea malipo,” Trump alisema kuhusu zaidi ya dola bilioni 100 za thamani ya zana za kijeshi ambazo Washington ilisafirisha huko Kyiv kuwasaidia wapiganaji wake.
Bila vifaa vyetu, alisema, vita hivyo vingemalizika kwa haraka, huku Russia ikiishinda Ukraine.
Forum