Jumatano, Vatican iliripoti kwamba afya ya Francis, mwenye umri wa miaka 88, ilikuwa imeimirika kwa kiwango kidogo
Vatican haijasema iwapo Francis bado yupo katika hali mbaya sana ya afya, japo ilisema Jumatano kwamba matatizo yaliyokuwa yanakumba figo yalisuluhishwa.
Papa Francis alilazwa hospitalini Februari 14 na hii ndio mara ya kwanza amelazwa hospitalini kwa muda mrefu.
Amekuwa na matatizo ya mapafu, na sehemu ya mapafu yake iliondolewa alipokuwa kijana.
Waumini wa katoliki wamekuwa wakikusanyika mjini Vatican na sehemu zingine duniani kumuombea Francis ambaye amekuwa Papa tangu mwaka 2013, baada ya Papa Benedict kujiuzulu.
Forum