Mkutano huo ni wa hivi punde katika msururu wa mikutano kati ya pande hizo mbili, ikiwemo mazungumzo ya simu mapema mwezi huu kati ya rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Russia Vladimir Putin.
Wiki iliyopita, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio na mwenzake wa Russia Sergey Lavrov walikutana na miongoni mwa maswala wanayojadiliana ni namna ya kurejesha uhusiano mwema kati ya Marekani na Russia
Baada ya mazungumzo hayo, Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema kwamba mazungumzo ya Riyadh yalifikia makubaliano ya kuunda mbinu ya kushauriana ili kushughulikia maswala yanayovuruga uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kwa lengo la kuboresha uhusiano wa kidiplomasia.
Uhusiano kati ya Marekani na Russia umekuwa mbaya kwa muda wa muongo uliopita, pande zote zikifukuza wanadiplomasia kutoka upande mwingine.
Forum