Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 30, 2025 Local time: 22:55

Wahamiaji wanaosubiri kufukuzwa nchini Marekani wapelekwa Guantanamo Bay


Waziri wa ulinzi wa Marekani Pete Hegseth akikutana na wanajeshi kwenye kambi la jeshi la wanamaji ya Guantanamo Bay, Februari 25, 2025.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Pete Hegseth akikutana na wanajeshi kwenye kambi la jeshi la wanamaji ya Guantanamo Bay, Februari 25, 2025.

Wahamiaji zaidi wanaotarajiwa kufukuzwa kutoka nchini Marekani waliwasili katika kituo cha kuwashikilia kwa muda cha Guantanamo Bay, nchini Cuba.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Pete Hegseth aliitembelea kambi ya jeshi la wanamaji ili kupata taarifa mpya kuhusu juhudi za kuwafukuza wahamiaji kwa wingi.

Ndege ya mizigo ya Marekani ikibeba wahamiaji tisa kutoka Fort Bliss huko Texas ilitua Guantanamo Bay Jumanne mchana, afisa wa wizara ya ulinzi aliiambia VOA.

Afisa wa pili alisema abiria hao wote tisa wanachukuliwa kama wahamiaji haramu hatari sana, na walipelekwa kwenye kituo hicho cha Guantanamo Bay.

Afisa wa tatu alisema ndege nyingine inayobeba wahamiaji zaidi inatarajiwa kuwasili huko leo Jumatano.

Maafisa wote hao wamezungumza na VOA kwa masharti ya kutotajwa majina kwa sababu hawaruhusiwe kuzungumzia operesheni za kuwafukuza wahamiaji.

Forum

XS
SM
MD
LG