Afisa wa Umoja wa Afrika ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliiambia VOA kwamba wanajeshi wa Burundi ambao wamekuwa nchini Somalia tangu 2007 wataondoka nchi humo baada ya serikali za nchi hizo mbili kushindwa kukubaliana kuhusu idadi ya wanajeshi kutoka Burundi.
Kikosi cha Umoja wa Afrika cha kusaidia katika juhudi za kurejesha amani nchini Somalia, au AUSSOM, kinatarajiwa kuwa na wanajeshi 11,900 ardhini nchini Somalia, wakiwemo wanajeshi, polisi na wafanyakazi raia , kulingana na maafisa wa Somalia na Umoja wa Afrika.
Mkataba huo mpya unasema kutakuwa na wanajeshi 4,500 kutoka Uganda, 2,500 kutoka Ethiopia, 1,520 kutoka Djibouti, 1,410 kutoka Kenya na 1,091 kutoka Misri, kulingana na maafisa hao.
Forum