Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia amesema maandalizi yameanza kwa mkutano wa ana kwa ana kati ya rais wa Marekani Donald Trump na Vladimir Putin wa Russia.
Rais wa Tunisia Kais Saied siku ya Jumamosi alitoa wito kwa sheria inayosimamia benki kuu kufanyiwa marekebisho, na hivyo kuzua wasiwasi kwamba benki hiyo itapoteza uhuru wake na uingiliaji wa moja kwa moja wa serikali katika sera za fedha.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na Rais wa Kenya William Ruto walihimiza kusitishwa kwa mapigano mara moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati wa mazungumzo yao ya simu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema Ijumaa.
Burundi inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu wakati zaidi ya watu elfu 40 wamekimbilia nchini humo katika kipindi cha wiki mbili wakitoroka vita mashariki mwa DRC, Umoja wa Mataifa umesema Ijumaa.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), Wafula Wanyonyi Chebukati, aliaga dunia jana Alhamisi katika hospitali moja mjini Nairobi akiwa na umri wa miaka 63, baada ya kuugua kwa muda mrefu, kama ilivyothibitishwa na familia yake.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Ijumaa kwamba Hamas italipa gharama kwa kushindwa kuuachilia mwili wa mateka Shiri Babas, kulingana na makubaliano ya amani na Israel.
Programu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNDP, kupitia ripoti mpya ya Alhamisi imesema kuwa huenda ikachukua takriban muongo mmoja kwa Syria kurejea kwenye viwango vya kiuchumi vya kabla ya vita, na kama kasi ndogo ya ukuaji iliyopo itaendelea, basi huenda ikachukua zaidi ya miaka 50.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Kristi Noem Alhamisi amepunguza muda wa kulinda wahamiaji dhidi ya kurejeshwa pamoja na kufuta vibali vya kufanya kazi kwa wahamiaji 521,000 wa Haiti waliokuwa chini ya mpango maalumu ikiwa na maana kwamba utamalizika Agosti, msemaji wa wizara hiyo amesema.
Juhudi za utawala wa Trump kuelekea kulainisha usalama wa taifa na idara za usalama Alhamisi zimepiga hatua muhimu baada ya wajumbe wa Seneti kupiga kura 51-49 za kuidhinisha Kash Patel kuwa mkuu wa Idara ya upelelezi ya Marekani, FBI.
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance aliongoza Mkutano wa Siasa wa kihafidhina na vikao vingine muhimu vinavyohusu Cryptocurrency
Viongozi wa Taliban wenye msimamo mkali nchini Afghanistan, wamekataa mamlaka ya mahakama ya uhalifu wa kimataifa ICC nchini humo, na kutangaza hatua ya waliokuwa viongozi wa nchi hiyo kuingiza Afghanistan katika makubaliano ya ICC mwaka 2003, kuwa kinyume cha sheria.
Pandisha zaidi