Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 16:29

Kash Patel aidhinishwa kama mkuu wa FBI


Kash Patel ambaye ameidhinishwa na Senate Alhamisi kuwa mkuu wa FBI.
Kash Patel ambaye ameidhinishwa na Senate Alhamisi kuwa mkuu wa FBI.

Juhudi za utawala wa Trump kuelekea kulainisha usalama wa taifa na idara za usalama Alhamisi zimepiga hatua muhimu baada ya wajumbe wa Seneti kupiga kura 51-49 za kuidhinisha Kash Patel kuwa mkuu wa Idara ya upelelezi ya Marekani, FBI.

Kura hiyo inamuweka Patel kwenye uongozi wa idara hiyo yenye nguvu, ambapo awali aliahidi kuleta mabadiliko wakati wakosoaji wa Rais wa Marekani Donald Trump wakisema kuwa utawala wake unahujumu utamaduni wa uhuru wa idara hiyo.

Warepablikan wawili –Seneta Susan Collins na Lisa Murkowski, walipiga kura na Wademokrat wakipinga kuidhinishwa kwa Patel. Hata hivyo uungaji mkono kutoka kwa Warepablikan wengine ulimpatia Patel ushindi mdogo, wengi wao wakimsifia na kusema kuwa ataleta mabadiliko.

“Wamarekani wengi katika miaka ya karibuni wamepoteza Imani yao kwa FBI, sababu kubwa ikiwa ni dhana kwamba siasa zimeingilia majukumu yake muhimu,” alisema kiongozi wa walio wengi kwenye Seneti John Thune, muda mfupi kabla ya kura ya Alhamisi kufanyika.

“Tunahitaji idara inayofanya kazi pamoja kushughulikia tishio dhidi ya nchi yetu,”Thune aliongeza kusema. Alisema kuwa yupo tayari kushirikiana na Patel ili kuhakikisha kuwa FBI inatekeleza majukumu yake ipasavyo. Baadhi ya Warepablikan wenzake pia wametoa maoni sawa na hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG