Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 01:56

Rais wa Tunisia Kais Saied atoa wito kwa sheria inayosimamia benki kuu kufanyiwa marekebisho


Rais wa Tunisia Kais Saied alipotoa hotuba katika hafla ya kuapishwa kwa serikali mpya katika Ikulu ya Carthage huko mji mkuu wa Tunis, Februari 27, 2020.
Rais wa Tunisia Kais Saied alipotoa hotuba katika hafla ya kuapishwa kwa serikali mpya katika Ikulu ya Carthage huko mji mkuu wa Tunis, Februari 27, 2020.

Rais wa Tunisia Kais Saied siku ya  Jumamosi alitoa wito kwa sheria inayosimamia benki kuu kufanyiwa marekebisho, na hivyo kuzua wasiwasi kwamba benki hiyo itapoteza uhuru wake na uingiliaji wa moja kwa moja wa serikali katika sera za fedha.

Saied alisema katika mkutano na Gavana wa benki kuu Zouhair Nouri kwamba ni wakati wa kubadilisha sheria ya mwaka 2016 ambayo iliipa benki mamlaka juu ya sera ya fedha, akiba na dhahabu.

"Tunataka benki kuu ya kitaifa, sio kama wengine walivyotaka iwe kulingana na maagizo kutoka nje," aliongeza, katika video iliyotolewa na ofisi ya rais.

Forum

XS
SM
MD
LG