Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Ijumaa kwamba Hamas italipa gharama kwa kushindwa kuuachilia mwili wa mateka Shiri Babas, kulingana na makubaliano ya amani na Israel.
Tutachukua hatua kwa nia ya kumrudisha Shiri nyumbani pamoja na mateka wetu wote walio hai na waliokufa na kuhakikisha Hamas inalipa gharama kamili kwa ukatili huu na uovu wa ukiukaji wa makubaliano, Netanyahu alisema katika taarifa ya kwenye video.
"Sio tu kwamba walimteka baba, Yarden Bibas, mama kijana, Shiri, Pamoja na watoto wao wawili wadogo kwa njia isiyofikirika lakini pia walishindwa kumrudisha Shiri kwa watoto wake wadogo, malaika wadogo, na badala yake waliuweka mwili wa mwanamke wa Gaza kwenye jeneza", alisema.
Hamas imesema Ijumaa kuwa mabaki ya Shiri Babas yalionekana kuchanganywa na mabaki mengine ya binadamu kutoka kwenye vifusi baada ya shambulio la anga la Israel kupiga eneo alilokuwa akishikiliwa, shirika la habari la Reuters iliripoti.
Forum