Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia amesema maandalizi yameanza kwa mkutano wa ana kwa ana kati ya rais wa Marekani Donald Trump na Vladimir Putin wa Russia.
Sergei Ryabkov aliviambia vyombo vya habari vya serikali ya Russia Jumamosi kwamba mkutano kama huo unaweza kuhusisha mazungumzo mapana kuhusu masuala ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na vita vya Ukraine.
Lakini alisema juhudi za kulifanikisha ziko katika hatua ya awali. Wiki iliyopita, wawakilishi wa Russia na Marekani walikubaliana kuanza mchakato wa kumaliza vita na kuboresha uhusiano wao wa kidiplomasia na kiuchumi, katika mazungumzo ya ngazi ya juu nchini Saudi Arabia ambayo yaliashiria hali ya kipekee katika sera za kigeni za Marekani chini ya Rais Trump.
Forum