Mkutano uliofanyika White House kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Ijumaa uliolenga kufikia makubaliano ambayo huenda yatairuhusu Marekani kupata haki ya madini nadra ya Ukraine uligeuka kuwa ni malumbano.
Waislamu sehemu mbali mbali duniani wanajitayarisha kuuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuangalia mwezi, kuanza ibada hadi ununuzi wa bidhaa za kutumia mwezi huu.
Maelfu ya watu walikusanyika katika miji kote Ugiriki siku ya Ijumaa kudai haki yao wakati wa kumbukumbu ya mwaka wa pili wa ajali mbaya zaidi ya treni kuwahi kutokea nchini humo, huku wafanyakazi waliogoma wakisimamisha safari za ndege na usafiri wa baharini na treni.
Mahakama ya Juu ya Namibia siku ya Ijumaa ilitupilia mbali pingamizi dhidi ya uchaguzi wa rais wa mwaka jana lililowasilishwa na vyama vya upinzani, hatua ambayo inampa nafasi Netumbo Nandi-Ndaitwah wa chama kinachotawala, kuwa rais kuanzia mwezi ujao.
Shirika la serikali ya Marekani linalosimamia vyombo vya habari vinavyorusha matangazo kote duniani, USAGM, Alhamisi limetangaza kuwa mwanahabari aliyegeuka mwanasiasa Kari Lake atajunga na shirika hilo kama mshauri maalum.
Watu 11 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa Alhamisi wakati wa mlipuko katika mji wa mashariki mwa Congo wa Bukavu uliotokea kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na viongozi wa kundi la M23, ambalo lilichukua udhibiti wa mji huo mapema mwezi huu.
Rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba ataweka ushuru wa asilimia 25 kwenye bidhaa kutoka Canada na Mexico wiki ijayo kama alivyopanga hapo awali, akidai kuwa nchi hizo mbili, Jirani za Mrekani, bado hazifanyi vya kutosha kuzuia dawa za kulevya kuingia Marekani.
Marekani na Uingereza zinajadiliana kuhusu mkataba wa kibiashara kati ya nchi mbili, Rais wa Marekani Donald Trump aliuambia mkutano wa waandishi wa habari Alhamishi akiwa pamoja na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer.
Australia imeahidi kuendelea kutoa msaada mkubwa kwa nchi za kusini mwa Pacific, katika mkutano kuhusu usalama na Uchumi, uliofanyika leo Alhamisi na Vanuatu wakati wa thathmini ya athari zinazoweza kutokea kufuatia hatua ya rais Donald Trump kupunguza msaada wa Marekani nje ya nchi.
Wanadiplomasia wa Marekani na Russia wamekutana leo alhamisi Istanbul kwa mazungumzo kuhusu utendakazi wa balozi zao mjini Moscow na Washington.
Vatican imesema kwamba kiongozi wa kanisa la katoliki Papa Francis, amelala vyema usiku wa kuamkia leo na kwamba alikuwa anapumzika, akiwa bado hospitalini mjini Rome ambapo anatibiwa homa ya mapafu.
Marekani itawekeza hadi dola bilioni 1 kukabiliana na kusambaa kwa mafua ya ndege, pamoja na kuongeza uagizaji wa mayai kutoka nje katika juhudi za kupunguza bei ghali ya bidhaa hiyo, waziri wa kilimo Brooke Rollins alisema Jumatano.
Pandisha zaidi