Trump alimtishia Zelenskyy “utaingia katika makubaliano au sisi tunatoka.”
Katika taarifa iliyobandikwa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia mkutano huo, Rais Trump aliashiria kuwa pendekezo la makubaliano halipo tena.
“Nimebaini kuwa Rais Zelenskyy hayuko tayari kwa Amani kama Marekani inahusika, kwasababu anahisi kuhusika kwetu kunampa fursa kubwa katika mashauriano,” Trump aliandika.
“Umeidharau Marekani katika ofisi yake ya Oval inayopendwa. Anasema kurudi akiwa tayari kwa Amani.”
Majibizano makali, yaliyoshuhudiwa na darzeni ya waandishi wa habari wa Marekani na Ukraine katika ofisi ya Oval, yalikuwa ya sauti ya ugomvi kwa karibu dakika 40 wakati Zelenskyy alizungumzia uvamizi wa Russia wa 2014 huko Crimea.
Makamu Rais wa Marekani JD Vance haraka alimkosoa Zelenskyy, akimshutumu kwa kujihusisha na “ziara za propaganda.”
“Nadhani ni dharau kwa wewe kuja Ofisi ya Oval kujaribu kushtaki hili mbele ya vyombo vya habari vya Marekani,” alimueleza Zelenskyy.
Wote Vance na Trump wamemshutumu kiongozi wa Ukraine kwa kutoshukuru kwa msaada kwa nchi yake ambao umetolewa na Washington.
“Huna karata za kucheza hivi sasa,” Trump alisema akipandisha sauti yake wakati Zelenskyy akijaribu kumkemea. “Unacheza kamari na maisha ya mamilioni ya watu. Unacheza kamari na Vita vya Tatu vya Dunia.”
Zelenskyy aliondoka White Houe mapema bila ya kushiriki mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.
Makubalino ya madini nadra
Kabla ya mkutano huo, Trump alisema alikuwa anakaribia kutia Saini mkataba huo na Zelenskyy.
“Tuna kitu ambacho ni makubaliano ya haki, na tunatazamia kuingia na kuchimba, kuchimba, kuchimba na kufanya kazi na kupata baadhi ya madini nadra ya ardhi,” Trump alimueleza Zelenskyy ambaye alionekana hakuwa na utulivu.
Makublaiano yalijumuisha vipengele kwa umiliki wa pamoja na utawala wa ufadhili wa ujenzi baada ya vita kwa Ukraine, ambapo Ukraine itatenga 50% ya mapato ya siku za usoni kutokana na rasilimali za asili za nchi hiyo.
Trump alielezea makubaliano hayo ya madini kama aina ya “mkataba” kutokana na dhamana ya ulinziambapo Marekani inaunga mkono jeshi la ulinzi wa amani la Ulaya nchini Ukraine baada ya vita vyake na Russia kumalizika.
“Ina maana tutaingia ndani, ni nia kubwa ya dhati kutoka kwa Marekani,” amesema.
Makubaliano hayo yanaeleza kuwa Marekani itadumisha “dhamira ya muda mrefu ya kifedha kwa maendeleo ya Ukraine.” Hairejelei moja kwa moja jitihada za kukomesha uvamizi wa Russia kwa Ukraine au kuhusu mipango ya usalama ya siku zijazo. “Serikali ya Marekani inaunga mkono jitihada za Ukraine kupata uhakikisho wa usalama unaohitajika ili kuanzisha amani ya kudumu.”
Mbali ya makubaliano ya madini, Trump hajatoa dhamana yoyote ya usalama kwa ulinzi wa amani wa Ulaya ili kuimarisha sitisho la mapigano kati ya Ukraine na Russia – madai yaliyotolewa na Ufaransa, Uingereza na washirika wengine wa NATO.
“Sitaki luzungumza kuhusu ulinzi wa amani mpaka tuwe na makublaiano,” Trump alisema wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer siku ya Alhamisi huko White House.
Mkutano wa Kwanza White House
Trump and Zelenskyy wamekuwa na mawasiliano kadhaa ya moja kwa moja katika siku zilizopita, lakini Ijumaa ni mkutano wao wa kanza uliofanyika White House. Mapema mwezi huu wawili hao walizungumza kwa simu, kufuatia mazungumzo ya simu ya Trump na Rais wa Russia Vladimir Putin.
Tangu aingie madarakani, Trump ameongeza shinikizo lake kwa Ukraine, akisema siyo kweli kuwa Kyiuv ilianzisha vita na Russia na kumuita Zelenskyy ‘dikteta”.
Pia amerejea dai kuwa Marekani imetua dola bilioni 350 katika vita vya Ukraine – idadi ambayo ni kubwa sana kurekodiwa na Wizara ya Ulinzi na kundi linalofuatilia matumkzi ya Marekani kwa Ukraine.
Wakati huo huo Trump anafuatilia mazungumzo ya moja kwa moja na Russia bila ya kuihusisha Kyiv au washirika wa Ulaya, akitetea wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kama ‘kitu cha kawaida’.
Forum